Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KIPIGO CHA MBWA MWIZI . YANGA NI BALAAAA.


Kipigo cha Kagera Sugar kutoka Yanga kilichoweka historia Kaitaba

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo Jumamosi ya October 22 2016 kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans imeendeleza harakati zake za kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu kwa kuvaana na Kagera Sugarkatika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Yanga leo wamecheza na Kagera Sugar katika uwanja wa nyasi bandia wa Kaitaba na kuandika historia ya kumfunga mwenyeji Kagera Sugar kwa goli 6-2, idadi ambayo imefanya ndio kuwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kufungana kwa idadi kubwa ya magoli kwa msimu wa 2016/2017.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4, 73, Simon Msuva dakika ya 20, Obrey Chirwa dakika ya 25, 63 na Deus Kaseke, magoli pekee ya Kagera Sugaryalifungwa na  Mbaraka Yusuph aliyefunga magoli mawili dakika ya 3 na 48, hiyo ndio mara ya kwanza kwa uwanja wa Kaitaba kufungwa goli nyingi katika mechi za Ligi Kuu toka uwekwe nyasi bandia.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
Powered by Blogger.
© Copyright COMEDY
Back To Top